JPM Amwaga Milioni 4 Hadharani!! Wakati Akizindua Kiwanda Igogo
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli leo Oktoba 31, 2017 amezindua Kiwanda cha
Victoria Moulders kilichopo eneo la Igogo jijini Mwanza ambacho
kinashughulika na utengenezaji wa vyombo vya plastiki na vifungashio vya
mifuko.
Akizungumza wakatio wa uzinduzi huo, Rais Magufuli amewapomgeza wamiliki
wa Kiwanda hicho ambacho kimetengeneza ajira kwa vijana zaidi ya 500
huku kikiwa kichocheo kikubwa cha ukuaji uchumi jijini humo kuendana na
mkatakati wa serikali ya Awamu ya tano ya kufufua na kukuza sekta ya
viwanda nchini.
"Ni jukumu letu kama taifa kuamua kusahihisha makosa au tuendelee na
makosa, Nyaza kulikuwa na viwanda kila mahali, baada ya mzee Masele
kuondoka viwanda vikapotea. Mzee Masele ndiye mtu peke aliyenichangia
shilingi elfu 10 kwenda kuchukua fomu ya ubunge.
"Kiwanda hiki kimewapa ajira zaidi ya vijana 500, kisingekuwepo pengine
wangekuwa majambazi. Nikupongeze waziri kwa utendaji wako na kuhakikisha
Tanzania ya Viwanda inawezekana," alisema Rais magufli.
Aidha Rais Magufuli amezichangia mifuko 200 ya saruji kwa shule mbili za
Kata ya Igogo ambapo kila shule itapewa mifuko 100. Pesa kiasi cha Sh.
Milioni 3 amezikabidhi kwa diwani wa kata hiyo na mbunge wake ili
watekeleze adhima ya kununua saruji za ujenzi wa shule hizo.
Pia amechangia pesa kiasi cha Sh. Milioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi
za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Igogo, ambazo amemkabidhi katibu
wa CCM Kata.
Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdate
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdate

Post a Comment