Yanga yaja kidijitali, yazindua kipindi chake cha TV (Press Conference - 20/03/2018)


Klabu ya Yanga leo imezindua rasmi kipindi chake cha televisheni kitakachokuwa kikiruka kupitia channel ya Azam Sports 2 inayopatikana ndani ya kisimbusi cha Azam TV.

 Zoezi hilo limefanyika leo makao makuu ya klabu hiyo, mbele ya Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa, Mkuu wa Idara ya habari na mawasiliano wa klabu hiyo Dismas Ten na Meneja wa Idara ya Michezo wa Azam Media, Baruan Muhuza.

 Viongozi hao kutoka pande zote mbili (Yanga na Azam TV) wamesaini makubaliano ya kurusha kipindi hicho kuanzia Jumanne tarehe 01 Aprili, 2018 na kitakwenda kwa jina la ‘Yanga TV’, mkataba huo ukiwa ni wa miaka mitatu.

 Akizungumzia kipindi hicho, Baruan Muhuza amesema kipindi hicho kitaandaliwa na Yanga wenyewe kwa zaidi ya asilimia 80, na asilimia 20 pekee ndiyo itakayokuwa chini ya Azam TV.

 Hii ni sehemu ya mkutano na wanahabari uliofanyika leo kuzungumzia suala hilo kabla ya kufanya uzinduzi rasmi.
SOURCE Azam TV


Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE 
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates

No comments

TUTUMIE UPDATES ZAKO KUPITIA
WhatsApp: +255 658 164282

Email: djchoka@gmail.com