DSTV waigharamikia harusi hii ya kifahari, Nandy na Aslay walitumbuiza, wazazi wadai ni muujiza

Kampuni ya DSTV kupitia kipindi chake cha Harusi Yetu kinachoonekana kwenye channel ya Maisha Magic Bongo, iliandaa shindano ambao maharusi watarajiwa walituma maombi kwaajili ya kuwania fursa adimu ya kugharamikiwa harusi yao. Maharusi wengi watarajiwa walituma maombi yao, lakini ni Solomon Asubi Mwaigwisya na Magreth Richard ndio walioshinda. Baada ya maandalizi makubwa, harusi yao imefanyika Jumamosi ya April 28, kwenye ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam na gharama zote zikiwa chini ya DSTV. Safari yao ya kuelekea siku hiyo ya harusi na siku yenyewe, itaoneshwa kwenye kipindi cha Harusi Yetu. Nandy na Aslay walitumbuiza kwenye usiku huo. Katika video hii, wazazi wa maharusi wamezungumza na SnS kuelezea hisia zao. Wanaoanza kuongea ni wazazi Bwana Harusi, Solomon, Mr and Mrs Mwaigwisya wakifuatiwa na wazazi wa Bi. Harusi, Magreth, Mr and Mrs Richard ambao makazi yao ni Arusha
SUBSCRIBE SimuliziNaSauti
Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdat
Post a Comment