"Mama alinipiga marufuku" – Irene
Mlimbwende Irene mwenye urembo wake wa haja ambaye alipata umaarufu kwa kuonekana kwenye video za wasanii wa bongo, amesema mama yake alimkataza kufanya kazi hiyo akihofia kupata matatizo kwa mtoto wake huyo.
Akipiga stori na Big Chawa wa Planet bongo ya East Africa Radio, Irene ambaye amesema mama yake hakutaka kabisa aonekane kwenye video, na hata alipomruhusu alimtaka aende na kaka yake ili kumlinda.
“Mama yangu alikuwa hataki, hapendi yaani basi nikakata tamaa nikasema sifanyi mama hataki, lakini nilipofuatwa tena nikamwambia mama nataka kufanya video, alikubali lakini akaniambia uende na kaka yako, ndio nikakubaliwa”, alisema Irene.
Irene aliendelea kusema kuwa alikuwa ana ndoto za kuwa mwanamitindo na kutokea kwenye video hizo, na mpaka sasa anafurahi kuona aliweza kutimiza ndoto yake hiyo.
SOURCE: http://www.eatv.tv
Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates


Post a Comment