Huyu Ndiye Rapa Aliyeacha Chuo IFM, Na Kujikita Kwenye Muziki

Kama umeshawahi kusikia au kuiona ngoma ya Astara Vaste na Garagasha, basi jina la Rapa Azma anayewakilisha Jiji la Mbeya, litakuwa siyo geni masikioni mwako, aliwahi kuacha chuo IFM, alipokuwa akisomea masomo ya uhasibu, ili aweze kupata muda wa kufatilia kazi zake za muziki. Azma ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayoitwa Kidedea, aliyorekodi nchini Kenya, amesema kuwa; “Baada ya kuona kazi zangu za muziki hazifanyi vizuri, nikaamua kusimamisha masomo yangu kwa muda ili nishughulike na muziki tu, nilivyojiridhisha kwamba sasa muziki wangu ni tishio mjini, nikarudi tena chuo na kuendelea na masomo, ambapo mwaka jana nimefanikiwa kumaliza. “Kwa kipindi nilichosimama chuo, nilihakikisha nautumia muda wangu vizuri kukuza muziki wangu, nimefanikiwa kuachia ngoma ya Kidedea ambayo nilirekodi nchini Kenya, lakini pia nimefanya kolabo na msanii mkubwa nchini Kenya anaitwa Gilad, ambayo itatoka hivi karibuni. Kwa sasa mashabiki wangu waendelee kuburudika na Kidedea,” amesema Azma.

Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE 
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdates/

No comments

TUTUMIE UPDATES ZAKO KUPITIA
WhatsApp: +255 658 164282

Email: djchoka@gmail.com