Alichokisema RUGE Baada ya Jengo la CLOUDS Kuwaka Moto!
SEHEMU ya jengo la kituo cha Clouds Media Group lililoko Mikocheni jijini Dar es Salaam limeungua moto leo ambapo Mkurugenzi wa Vipindi wa kituo hicho, Ruge Mutahaba, amesema moto huo ulitokea bila ya mtu yeyote kuwa na taarifa nao ambapo ulianzia katika studio ndogo ya kurekodia. Aliongeza kwamba kituo hicho si mara ya kwanza kupatwa majanga ya moto ambapo mara ya kwanza walipokuwa katika jengo la Kitegauchumi eneo la Posta jijini Dar es Salaam, moto uliteketeza studio zao na kupoteza vitu mbalimbali ambapo moto wa leo umeteketeza baadhi ya ofisi za studio ya Televisheni. Hata hivyo, alikishukuru kikosi cha Zimamoto kwa kufika haraka eneo la tukio na kuuzima moto huo. Vilevile alisema hakuna binadamu aliyepata madhara kutokana na tukio hilo. Mutahaba alisema juhudi zaidi zinaendelea katika kituo hicho ili kurekebisha mambo yaliyotokea na kwamba ratiba zao zitaendelea kama kawaida.
SOURCE: Global TV Online
Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdate
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdate
Post a Comment