BAADA ya Raundi ya 10 kwa Msimamo Huu wa Ligi Kuu Nani ni Nani......?
Raundi ya kumi ya Ligi Kuu Bara msimu huu ilimalizika wikiendi iliyopita baada ya timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo kushuka katika viwanja tofauti kwa ajili ya kusaka pointi. Timu ya Simba ilifanikiwa kuendelea kuwa juu katika msimamo wa ligi hiyo baada kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya. Ushindi huo uliiwezesha timu hiyo kufikisha pointi 22 sawa na Azam FC ambayo pia ilifikisha pointi hizo baada ya kuifunga Njombe Mji bao 1-0. Hata hivyo, Simba inaongoza ligi hiyo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Yanga nayo ilijiimarisha katika nafasi yake ya tatu baada ya kuitandika Mbaye City mabao 5-0 na kufikisha pointi 20, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Wageni wa ligi hiyo, Singida United, nao walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli FC, huku Ruvu Shooting ikipata ushindi wake wa kwanza msimu huu kwa kuifunga Ndanda bao 1-0, wakati Majimaji ikiifunga Mbao FC mabao 2-1. Kagera Sugar nayo ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya ndugu zao Mtibwa Sugar ambayo tangu kuanza kwa msimu huu ilikuwa haijapoteza hata mchezo mmoja. Nao ndugu wawili wa mkoani Shinyanga, Stand United na Mwadui FC, walitoka uwanjani wakiwa hawajafungana.
SUBSCRIBE: Global TV Online
Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdat
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdat
Post a Comment