(Video) CHEKI DKT SHIKA ALIVYOPOKELEWA KAMA MFALME KAHAMA!


DKT Louis Shika ambaye amekuwa maarufu kwa muda mfupi kama ‘bilionea wa nyumba za Lugumi’ wakati wa kunadi nyumba za Said Lugumi jijini Dar es Salaam, ametunukiwa heshima ya kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya Chuo cha Sayansi ya Dawa kilichoko Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, ambako amepokelewa kama mfalme. Mapokezi hayo ya kipekee yameanzia uwanja wa ndege wa mjini Kahama alipowekwa kwenye gari la wazi huku msafara mkubwa uliokuwepo ukijumuisha na bodaboda, magari na mamia ya watu mbalimbali waliojitokeza kumwoma na kumlaki. Ziara hiyo ya Dkt. Shika mkoani humo itamalizika jioni hii chuoni hapo ambapo anatarajiwa kurejea kwa ndege Dar es Salaam usiku.


Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE 
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdat

No comments

TUTUMIE UPDATES ZAKO KUPITIA
WhatsApp: +255 658 164282

Email: djchoka@gmail.com