Bomba la Gesi Lalipuka Buguruni, Moto wa Kutisha!


Bomba la Gesi Lalipuka Buguruni, Moto wa Kutisha! MOTO mkubwa unaodaiwa kuwa ni wa gesi umelipuka na kuteketeza jengo eneo la Hospitali ya Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam jioni hii. Kikosi cha kuzima moto kimefika eneo la tukio na kinafanya kila juhudi za kuuzima moto huo ambao unaonekana kusambaa kwa kasi ambapo moto huo umesababisha magari na treni kushindwa kupita eneo hilo, chanzo kimedaiwa ni kupasuka kwa bomba la gesi.

Inasemekana bomba la gesi limepasuka na kusababisha moto mkubwa uliozua taharuki kwa wakazi na wafanyabiashara wanaozunguka eneo la Buguruni Mnyamani. Taarifa za awali za zinasema bomba hilo limelipuka baada ya wafanyakazi wa Dawasco kulitoboa kwa bahati mbaya wakati wakitengeneza bomba la maji. Madhara yaliyosabaishwa na moto huo ni kuteketea kwa baadhi ya vibanda vya wafanyabiashara, kuungua kwa nguzo za Tanesco na nyumba moja imeteketea kabisa.



Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE 
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdat

No comments

TUTUMIE UPDATES ZAKO KUPITIA
WhatsApp: +255 658 164282

Email: djchoka@gmail.com