PICHA: FLAVIANA MATATA agawa madarasa mawili ya shule ya msingi KIWANGWA-BAGAMOYO
Mwanamitindo wa Kimataifa afanyae kazi zake nchini Marekani,
Flaviana Matata kushoto akikabidhi mipira kwa wanaafunzi wa shule hiyo,
Flaviana ni mlezi wa shule hiyo.
|
Mwanamitindo Flaviana akionesha cheti cha heshima
alichotunukiwa na uongozi wa kata ya Chiwangwa baada ya kuwajengea majengo ya
shule.
|
Flaviana akiwahoji wanafunzi hao maendeleo yao ya masomo
shuleni hapo.
|
Flaviana akipokea cheti cha heshima kutokea kwa Mtendaji wa Kijiji
cha Msinune, Memory Mbangwa cha kutambua mchango wake huo.
|
Flaviana akiwa na watendaji wa kijiji hicho na kata pamoja
na wanakijiji waliojitokeza siku hiyo.
|
Alipata wasaha wa kupiga picha na wanafunzi pia siku hiyo ambao walimpongeza
kwa msaada wake huo
|
Na Evance Ng'ingo
MWANAMITINDO wa kimataifa afanyaye shughuli zake nchini
Marekani, Flaviana Matata madarasa mawili ya shule za msingi iliyopo katika
kijiji cha Msinune kilichopo kata ya Kiwangwa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
Flaviana alipewa jukumu la ulezi wa shule hiyo na wanakijiji
wa Msinune mwaka 2014 wakati alipoenda kuwasaidia wanafunzi mabegi ya shule,
walimpatia jukumu la kuwatengenezea vyoo, ofisi na nyumba za walimu pamoja na
kumalizia ujenzi wa darasa.
Tangia alipopewa majukumu hayo alianza kwa ujenzi wa vyoo
vya walimu na wanafunzi, na juzi alienda kukabidhi jengo la madarasa, darasa la
saba na la sita pamoja na ofisi ya Mkuu wa Shule.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Flaviana alisema,
tangia alipopewa jukumu la ulezi wa shule hiyo amekuwa akihangaika huku na kule
kupata fedha za kutatua kero za shule hiyo.
Alisema, kwa kufanikiwa kukabidhi jengo hio la madarasa
anaona kuwa ameshiriki kikamilifu katika kutekeleza jukumu lake kama mwanajamii
la kusaidia maendeleo ya elimu kwa jamii iliyokuwa na uhitaji mkubwa.
Alisema" sisi kama vijana kama watanzania tunalo jukumu
la kujitokeza na kusaidia maendeleo ya elimu na sekta nyingine muhimu nchini kwa
kuwa hili sio jukumu la serikali peke yake, sasa nimeshatengeneza vyoo vya
walimu na wanafunzi na leo nakabidhi darasa"
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Alex Lugaigalila
alisema ujenzi wa darasa huo utawaongezea ufanisi wanafunzi katika masomo yao
huku akibainisha wazi ushiriki wa Flaviana kwenye maendeleo ya shule hiyo
umeongeza hamasa ya wanafunzi kusoma.
Kwa upande wake Afisa wa elimu wa Kata hiyo,Blasius Alphonce
alisema kwa ujenzi wa jengo hilo, Flaviana amesaidia jitihada za serikali katika
kuendeleza elimu kwenye kata hiyo yenye vijiji vitano.
Jengo hilo la darasa lililojengwa lina vyumba viwili vikubwa
vilivyoezekwa kwa bati huku likuwa na madirisha makubwa yanayowezesha kupitisha
hewa na chumba cha mwalimu mkuu.
Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdat
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdat
Post a Comment