LIVE: JPM Akizindua Ukuta wa Mirerani Manyara


Rais John Pombe Magufuli, anazindua ukuta wa kuzuia kutoroshwa kwa madini ya Tanzanite, Mirerani jijini Arusha. Katika shughuli hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti alianza kwa kuwatambulisha viongozi mbalimbali wa serikali kisha Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Martini Busungu akatoa taarifa ya ujenzi wa ukuta huo.

 Gharama za ujenzi wa mradi huo ni Shilingi bilioni 5.6 na umejengwa na vijana wa JKT. Pia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mabeyo, amezungumza na kusema ukuta huo wenye urefu wa kilomita 24.5, ulianza kujengwa mwezi Novemba mwaka 2017 na kukamilika mwezi Februari mwaka 2018.

 Pia amesema maagizo ya ujenzi wa ukuta katika uwanja vita wa Ngerengere nao unajengwa na upo katika hatua za mwisho, ukuta huo una urefu wa kilometa 14 na wanaoshiriki katika ujenzi huo ni vijana waliojenga ukuta wa Mererani.

Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE 
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates

No comments

TUTUMIE UPDATES ZAKO KUPITIA
WhatsApp: +255 658 164282

Email: djchoka@gmail.com