Masogange Ameachiwa Huru!
Muda mfupi baada Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumhukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Tsh. Milioni 1.5, msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kwa kosa la kutumia madawa ya kulevya aina ya heroin, hatimaye imemuachia huru baada ya kulipa faini aliyotajiwa. Msanii huyo alikamatwa na polisi usiku wa kuamkia Februari 15, 2017, akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya. Masogange alikuwa miongoni mwa watu maarufu waliotajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati akipambana na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
SOURCE Global TV Online
Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdat
Post a Comment