ANAYEMDAI SHILOLE! "Narudi Mahakamani, Shilole ni Mshamba!

Ikiwa leo Machi 7, 2018 ndiyo siku ambayo msanii wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed 'Shilole', alitakiwa kutii amri ya Mahakama ya kumlipa mfanyabiashara Marry Musa, pesa taslimu shilingi Mil 14, ikiwa ni sehemu ya faini kutokana na hasara aliyomsababishia baada ya kutotokea kwenye shoo iliyokuwa imeandaliwa na mwanamama huyo licha ya kwamba alikuwa ameshamkamilishia malipo yake waliyokubaliana ya kiasi cha shilingi MIL 3.
Mfanyabiashara huyo Marry Musa, ameibuka na kuzungumza na Global Tv, na kusema kuwa tangu siku waliyotoka mahakamani Shilole hajamtafuta na kuzungumza naye chochote, na kwakuwa alitakiwa kumlipa leo na hajamlipa chochote kesho Alhamisi ya Machi 8 anatarajia kurudi tena mahakamani kujua hatma yake.
Aidha Mwanadada huyo amemshauri staa huyo wa ngoma ya Kigori, kuwa na lugha rafiki kwa kila mtu na aache kujiona kwamba yeye ni msela sana.
SOURCE Global TV Online
Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates
FACEBOOK FANS PAGE>>> https://www.facebook.com/djchokaupdat
Post a Comment