Mtanzania "Sensei Fundi Rumadha (4th Dan) Yondan" Apandishwa cheo na baraza la Karate Duniani
![]() |
| Sensei Kinjo, Gima, Yoshihiro Kancho Miyazato, sensei Fundi Rumadha na Sensei Rony Kluger toka Israel. Katika where za kupandiswa ngazi walimu kadhaa. |
![]() |
| Masensei toka Ujerumani, Ureno, Uingereza, Japan, na Tanzania katika semina "Gasshuku" wakiwa na furaha nyingi. |
MASTER MIYAZATO KANCHO WA OKINAWA
AMPANDISHA NGAZI SENSEI
FUNDI RUMADHA.(MTANZANIA
Masters
au walimu wakuu wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu Karate-Do chini
ya usimamizi wa mwenye kiti wake mkuu duniani, aliwafanyia mitihani ya
mikanda myeusi zaidi ya walimu 15 toka nga ya pili" Nidan" hadi ngazi ya
saba "Nanadan". Ngazi hizi zote kwa uramaduni wa mtindo huu wa Okinawa
Goju Ryu huchukua miaka mingi sana kupandiswa ngazi kulinganusha na
mitindo mingine.
Kongamano
la Karate mtindo wa Goju Ryu katika chama cha Jundokan So Honbu
hufanyika kila mwaka nchi za ulaya kwa kutembelewa na wakuu wake toka
katika visiwa vya Okinawa kuwasahihisha mbinu za mafunzo na mikakati
mipya ya chama na hatimae sasa kuwaalika walimu toka nje ya bara la
ulaya kwa muda wa miaka zaidi ya miwili sasa ikiwemo Tanzania na Angola.
Mwaka
huu, wakuu wapatao watano chini ya mwenye kiti sensei Yoshihiro
"Kancho" Miyazato, Tetsu Gima sensei, Tsuneo Kinjo sensei na Miyazaki
sensei na mjumbe mwingine pia. Wakuu wa Okinawa Goju, wametilia mkazo
na msisitizo mkubwa sana kwa kuzimudu mbinu kwa kina na matuzi yake, na
pia watoto wadogo kwani ndio walimu wa kesho.
Mengi
juu la misafara hii nikuwajumuisha masensei wote wa chama cha Jundokan
So Honbu, kuwasahihisha na kuwafundisha ngazi kwa wana Swahili kufanyiwa
hivyo, kulikoni kufanya gharama za kwenda Okinawa, Japan kimafunzo.
Sensei
Fundi Rumadha aliweza kufanya mitihani wake toka Dan ya tatu "Sandan"
kwenda ngazi ya nne "Yondan" na kufauli vizuri chini ya waamuzi masters
toka Okinawa chini
ya
Miyazato sensei. Sensei Fundi Rumadha amepewa mamlaka kuwasaidia
wanafunzi wake wa Tanzania, kuwafanyia mitihani na kuwapa "Dan" hadi
ngazi ya pili " Nidan" sababu chama chake kuanzia Dan ya 3 hutolewa na
Master Miyazato pekee hadi leo hii.
Nimatumai
yetu wanachama wa Jundokan So Honbu Tanzania kujiwajibisha kimafunzo,
na kuimarisha umadhubuti wa mbinu" Techniques" kulikoni kulenga sana
ngazi bila msingi mazuri kimafunzo, hasa katika kufanya "Kata" na
"Bunkai".
Sensei
Fundi Rumadha ingawa sasa anashikilia ngazi ya daraja la nne "Yondan",
na umahili wake wa Karate kwa zaidi ya miaka 38, alitoa Shukran zake kwa
mlezi wake wa mafunzi tokea utotoni, mwalimu "Sensei Magoma N. Sarya
chini ya uongozi wake "Bomani Brigade" kama ilivyojilikana "BB" na
mwanzilishi hayati Nantambu Camara Bomani sensei, mwanzilishi wa Okinawa
Goju Ryu Tanzania 1973.
Tanzania
na Angola zinatarajia kuhudhuria maadhimisho ya miaka 65 tangu
kuanzishwa kwa chama cha "Jundokan" na Master Eiichi Miyazato sensei
huko Naha City, Okinawa mwezi wa Novemba 1918, kwa sasa kinaongozwa na
mwanae Yoshihiro Kancho Miyazato.
www.instagram.com/fundi_romi
www.instagram.com/fundi_romi




Post a Comment