PENALTI ya Mkude Iliyowainua Simba VS K Sharks


Hatimaye klabu ya Simba imefunguka na kusema fedha zote za ubingwa wa Sports Pesa Super Cup watapewa wachezaji. Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema fedha zote dola 30,000 (zaidi ya Sh milioni 66) kama watabeba ubingwa zitakuwa mali ya wachezaji. “Tayari tumezungumza nao na kuwaeleza kuhisiana na suala hilo kwamba fedha zote zitaenda kwao,” alisema. Manara amesema hayo mara tu baada ya Simba kushinda kwa mikwaju ya penalti na kutinga nusu fainali. Simba imeing’oa Kariobang Sharks kwa penalti 3-2 baada ya mechi kwisha bila bao katika dakika 90.

Download DJChokaUpDates Android Application Click >>> HERE 
TWITTER @DJChokaUpDates
INSTAGRAM @DJChokaUpDates

No comments

TUTUMIE UPDATES ZAKO KUPITIA
WhatsApp: +255 658 164282

Email: djchoka@gmail.com